Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli Mwigulu alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo, alizungumza na maafisa na askari Uhamiaji na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kulia) alipokuwa anatoa hotuba fupi na baadaye kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na maafisa na askari wa Uhamiaji wa Makao Makuu wa Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Waziri Mwigulu aliwataka askari hao waongeze juhudi zaidi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua kali bila kuwaonea watu katika ukamataji wao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (aliyevaa tai) na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli wakitoka moja ya nyumba zinazojengwa kwa ajili ya Makamishna wa Uhamiaji, Kijichi, jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu alizikagua nyumba hizo ambazo zipo hatua za mwisho kukamilika. Waziri huyo alifanya ziara katika idara hiyo kwa kutembelea maeneo ya utendaji katika ofisi hizo na baadaye alitembelea mradi wa nyumba za Makamishna na Kiwanda cha Uchapishaji Nyaraka za Uhamiaji, zilizopo Kijichi jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...