THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Ndama mtoto wa Ng'ombe matatani


Mfanya biashara maarufu jijini Dar es salaam Ndama Hussein maarufu kama Ndama mtoto wa Ng’ombe (pichani) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita ikiwamo kughushi na kutakatisha Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh, bilioni 1.181). 

Ndama Mtoto wa Ng'ombe  alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.  Upande wa Jamhuri ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Leonard Challo.
 Wakili Msigwa alidai kuwa Februari 20, mwaka 2014, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na lengo la kudanganya alighushi nyaraka za kusafirisha madini akionyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited imepewa kibali cha kusafirisha boksi nne za vipande wa dhahabu zenye uzito wa kilo 207 zenye thamani ya Dola za Kimarekani 8.2 kwa Kampuni yenye makazi yake nchini Austaria inayojulikana kama Trade TJL DTYL Limited huku akijua nyaraka hizo za uongo. 
 Katika shtaka la pili, Machi 6, mwaka 2014, jijini Dar es Salaam akiwa na nia ya kudanganya, Ndama Mtoto wa Ng'ombe aliandaa nyaraka za uongo kuonyesha kwamba hati ya kuondolea mizigo kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa za tarehe hiyo, akiwa na lengo la kuonyesha kwamba vipande vya dhahabu vyenye uzito wa kilo 207 kutoka Jamhuri ya Congo, kuwa zinasafirishwa na Kampuni ya Muru Platnum kwenda Austraria. 
Wakili  Msigwa alidai katika shtaka la tatu, Februari 20, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kudanganya alighushi nyaraka zikionyesha kuwa ni fomu ya tamko la kodi akionyesha Kampuni ya Muru Platnum imelipa Dola za Kimarekani 331,200 kama kodi ya kuingiza mzigo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kilo 207 ya vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku akijua ni uongo. 
Katika shtaka nne, Februari 20, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka zauongo za kuonyesha kuwa ni za bima kutoka Kampuni ya Phoenix Ltd za terehe hiyo, akilenga kuonyesha kwamba Kampuni ya Muru Platnum imekatia bima boksi nne za vipande vya dhahabu zenye uzito wa kilo 207 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 huku akijua ni uongo. 
 Katika shtaka la tano na sita, kati ya Februari 26 na Machi 3, mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, alijipatia kwa njia ya uongo na kutakatisha Dola za Kimarekani, 540,390 (sawa na Sh. Bilioni 1.181) kutoka Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited kwa madai kuwa angesambaza na kusafirisha nje ya nchi kilo 207 za vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 lakini hakufanya hivyo. 
 Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitakatisha fedha hizo zilizopatikana kwa njia ya jinai kwa kuelekeza kiasi hicho cha fedha kuingizwa katika akaunti iliyopo benki ya Stanbic yenye jina la Kampuni ya Muru Platnum na baadaye alizitoa zote na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi huku akijua zimepatikana kwa njia ya udanganyifu. 
 Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na uliomba mahakama tarehe nyingine ya kutajwa. 
 Hakimu Nongwa alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 13, mwaka huu. Mshtakiwa alirudhishwa mahabusu kwa sababu mashtaka ya kutakatisha fedha hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    HAKUNA MWANZO HUSIO KUWA NA MWISHO, MTU UMEISHA KUWA NA MAISHA YAKO MAZURI, KWA NINI? USIACHE HAYO MAMBO MUDA MREFU?

    DR, JAMESY