THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NG’OMBE TATU NA MBUZI TATU ZATOLEWA KWA MABINGWA WA KATA ZOTE ZA TARAFA YA SADAN KWENYE MASHINDANO YA MGIMWA CUPNa Fredy Mgunda,Mafinga

MASHINDANO ya Mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa yanayojulikana kama Mgimwa Cup yamefika tamati katika tarafa ya Sadan yenye kata tatu ambazo Ikwea,Sadan na Igombavanu na fainali zote zilifanyika katika kata husika ambapo kila mshindi wa kata alipata ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipata mbuzi moja,hivyo jumla ya ng’ombe tatu na mbuzi tatu zimetolewa katika tarafa ya Sada.

Katika fainali ya kwanza ilichezwa katika viwanja vya kijiji cha Ugenza iliyopo katika kata ya Ikwea ilishuhudiwa timu ya Ugenza FC wakiibamiza timu ya Ikwea FC kwa goli 1-0 katika mchezo wa vuta nikuvute.

Baada ya mchezo huo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa michuano hiyo ambapo mshindi wa tatu ambaye ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa mipira miwili, mshindi wa pili Ikwea FC walipata mbuzi mmoja na mpira mmoja na mshindi wa kwanza ambaye ni Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mtenga aliwaasa wachezaji kuithamini michezo kwa kuwa sasa ni ajira hivyo wanajukumu la kujituma na kuipa kipaumbe michezo na kuacha tabia za kukaa kwenye vijiwe na vilabu ambako wanapoteza muda kwa kujadili mambo yasiyo ya msingi.Akifunga mashindano hayo mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba vijana hao wajiunge katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga wakifuatila mchezo wa fainali katika kata ya Ikwea ambapo mshindi alipata ng'ombe mmoja na mshindi wa pili akipokea zawdi ya mbuzi mmoja ambapo zawadi zote hizo zimetolewa na mbunge huyo. 
katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga akikabidhi ng'ombe kwa mshindi wa kwanza katika kata ya Ikwea ambapo mshindi wa kwanza ilikuwa timu ya Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga walipomkabidhi zawadi mshindi wa pili Ikwea FC mbuzi mmoja na mpira mmoja.