BENKI ya NMB imetoa msaada wa madawati 3500 kwa serikali yenye thamani ya sh. Bilioni 1.5 ya madawati yote ambayo walikuwa wameahidi kutoa tangu 2014 ikiwa ni jitihada ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa madawati, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene amesema benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia katika elimu.

Simbachawene amesema kuwa madawati hayo yatapelekwa katika mikoa ambayo haijaweza kumaliza tatizo la madawati ya kwa baadhi ya shule.

Amesema kuwa kuna baadhi ya mikoa imemaliza tatizo la madawati hivyo kutokana na msaada huo utasaidia sehemu kubwa kumaliza tatizo la madawati.

Madawati hayo yatakwenda katika shule za msingi na sekondari 71 kwa kila shule kupata madawati 50.

“Nashukuru kwa msaada huu katika mapambano ya upungufu wa madawati nchini,  baada ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuagiza ya kuwa hakuna mwanafunzi kukaa  chini tumefanikiwa na kubakiza wilaya chache ambapo madawati haya yatakwenda” amesema Simbachawene.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea madawati kutoka NMB leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene akipokea msaada wa madawati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene akikagua madawati aliyokabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...