THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NSSF YAENDELEA KUKAMILISHA MRADI WA JENGO LA MZIZIMA TOWERS

Na Anthony John blog Jamii.

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekamilisha mradi wa Jengo refu Afrika Mashariki-Mzizima Tower lililopo barabara ya  Azikiwe na Mkwepu Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Shirika hilo,Mkurugenzi wa Shirika hilo Prof. Godius Kahyarara  amesema Jengo hilo lipo hatua za mwisho za ukamilishaji wa ujenzi ambalo litakuwa na ghorofa 30 za makazi na 32 za Biashara.

Pia amesema Jengo hilo litakuwa na hoteli ya Nyota 5 na nyumba za makazi kwa ajili ya kuuza na kupangisha,Jengo linatarajiwa kukamilika mwakani 2017.Aidha Shilika hilo limesaini makubaliano na atakayekuwa muendeshaji wa Hoteli hiyo itakayokuwa katika Jengo la Mzizima na kutarajiwa kuanza kazi Mara moja baada ya Hoteli hiyo kufunguliwa.

"Baadhi ya miladi imekamilika na mengine ipo katika hatua za ukamilishwaji,NSSF inafungua rasmii upangishwaji wa litakalo kuwa Jengo refu Afrika Mashariki Mzizima Touwers" hayo amesema Kahyarara.
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF,Prof. Godius Kahyarara akizungumza na Waandishi kuhusiana na mradi wa Jengo la NSSF (Mzizima Tower) .

Baadhi ya Watumishi wa Shirika hilo wakiwa katika picha ya pamoja.