Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeshiriki katika kongamano la kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda, kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akiongea kwa niaba ya wadhamini wa kongamano hilo, Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, alisema NSSF kama sehemu ya jamii inao wajibu wa kushiriki katika uendelezaji wa viwanda kwa kuwa uelekeo huo utazalisha ajira nyingi ambapo waajiriwa hao watakuwa wanachama wa mfuko wa NSSF na itapata michango na kuiwekeza na baadae kuilipa kama Pensheni pindi ajira zao zitakapokoma.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akitoa mada wakati wa kongamano la siku mbili la wanataaluma kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda na mageuzi ya jamii. Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Nkurumah jijini Dar es Salaam jana na kudhaminiwa na NSSF. Kushoto ni Prof. Sam Maghimbi. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara na Prof. Sam Maghimbi (kushoto), wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko na Uhusino, Anna Nguzo (kulia), kuhusu mwamko wa wanachuo kujiunga na NSSF baada ya kupata elimu ya mafao yanayotolewayo na NSSf. Wanachuo wanaweza kujiunga na NSSF kupitia Scheme ya AA PLUS (Afya na Akiba kwa Wanachuo).  Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kujiunga na NSSF wakati wa kongamano la siku mbili la wanataaluma kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda na mageuzi ya Jamii. Kongamano hilo limedhamiwa na NSSF.
Wanachuo na wadau wakiwa katika kongamano hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...