THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NSSF YAWAONDOA WAPANGAJI WALIOSHINDWA KULIPA KATIKA NYUMBA ZA KIJICHI

Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu. 
Wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba na kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.
Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni Kijichi ambapo alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa  saba.
“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.
Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.
Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.
Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje na kupata hasara.