TIMU ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya askari magereza wa mkoani Mbeya Tanzania Prisons na kufikisha jumla ya alama 30 wakiwa nyuma ya alama tano dhdi ya mahasimu wao wakubwa Simba ambao wamepoteza mchezo wao wa leo. 
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ulikuwa wa kasi na kila upande ukicheza kwa umakini uliweza kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza huku kila timu ikiwa haijaona lango la mwenzake. 
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko na kuanza kulisakama lango la Tanzania Prisons lakini makosa ya washambuliaji wa timu hiyo walishindwa kutumia nafasi hizo na kukosa magoli, lakini makosa ya mabeki wa Yanga yalisabababisha Prisons kupata penati lakini uwezo wa golikipa Beno Kakolanya aliweza kuokoa mkwaju huo.
Mnamo dakika ya 74 mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga aliipatia Yanga penati inayopigwa na Simon Msuva na kuiandikia Yanga goli la kuongoza na mpaka dakika 90 za kumalizika kwa mchezaji huo.


Saimon Msuva Akitimuwa Vumbi kwa shuti kali wakati akipiga penati katika lango la Tanzania Prison na kuipatia yanga goli moja kwa bila katika mchezo ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya Ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Ya Soka Vodacom Tanzania Bara.

Haruna Niyonzima wa Timu ya Yanga Akimuomba Radhi Mchezaji Mwenzie Wa Timu ya Yanga Saimon Msuva  alipokuwa Akijibizana Na Muamuzi. 
Victor Hangaya Shoto Akimpoteza Deus Kaseke.
Kutoka Shoto ni Benjamin Asukile akichuana Vikali na Mwinyi Haji katika mtanange wa Yanga na Tanzania Prison ulio chezwa Katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
PICHA NA MR.PENGO MAELEZO ZAINAB NYAMKA MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...