NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya Temeke, walijiunga na mpango huo.
Katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7, 2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.
Akizungumza baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda, litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.
“Tunatoa wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda, machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.
 Baadhi ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pnsheni wa PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, Novemba 7, 2016.
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.
 Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...