THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

PROF. MUHONGO AKUTANA NA BODI NA MENEJIMENTI YA TPDC

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo amekutana na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika kikao kilichochadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na shirika hilo ikiwemo Mradi wa Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Katika kikao hicho Prof. Muhongo ameitaka Bodi na Menejimenti hiyo kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi husika kutokana na manufaa ya miradi hiyo kwa Maendeleo ya Taifa.

Mbali na Bodi na Menejimenti ya TPDC, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, wakati huo huo, Waziri Muhongo pia amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu sekta ya nishati ikiwemo chanzo cha Nishati Jadidifu.Pia, Waziri Muhongo amekutana na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza Jambo wakati wa Kikao chake na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Sehemu ya Menejimenti ya TPDC wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke (wa pili kushoto) na ujumbe uliofuatana na Balozi huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooken (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake walipomtembelea leo ofisini kwake Jijijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati Naibu Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.