Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amesema kuwa taifa lipo katika changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa linajenga, kukuza na kusimamia maadili kwa jamii nzima hasa kwa vijana waliopo mashuleni.

Profesa Ndalichako amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua  mdahalo kuhusu kujenga na kukuza maadili ,haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

“maadili na makuzi kwa vijana hasa wanafunzi ni suala linalopewa kipaumbelena serikali ya awamu ya tano hivyo nina imani mdahalo huu umeandaliwa kuzingatia dhana ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala mbalimbali hivyo wanafunzi msirudi nyuma” amesema Profesa Ndalichako.

Ameongeza kuwa suala la kujenga,kukuza na Kusimamia maadili siyo jukumu la Rais peke yake au tasisi moja  tu,viongozi wa Dini na jamii nzima hivyo sote tunapaswa kushirikiana kwa pamoja katika ngazi zote kuanzi mashuleni hadi mtaani.

Amasema kuwa jamii yetu imeshuhudia katika kipindi hiki kuwepo kwa viashiria vingi vinavyoonyesha kuporomoka kwa maadili kama hivyo dalili sio njema hata kidogo kwa mstakabali mzuri wa Taifa letu.

Alimaliza kwa kusema kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu hufundishika na Yule asiyetii hawezi kufundishika kwa kuwa hawawezi kusikiliza anachofundishika kwa kuwa hawezi kusikiliza anachofundishwa na Mwalimu ambaye ndio chachu ya mafanikio yake kitaaluma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameongozana na Mkurugenzi mkuu wa Tasisi kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola kuingia katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam.
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi ,Profesa Joyce Ndalichakoakizungumza wakati wa ufungzui wa madahalo wa kuhus maadili kwa wanafunzi.
baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wakifatilia kwa makini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...