Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akiwa na Profesa Chris Maina Peter aliyesimama pamoja na baadhi ya Maofisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania mara baada ya kutangazwa kwa majina ya wagombea 34 ambao walishinda kwa kupigiwa kura ya siri na Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa wajumbe wa Tume ya Kimataifa ya Sheria ( ILC) katika uchaguzi uliofanyika jana ( alhamisi) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.
Bi. Lilian Mukasa ,Afisa wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambaye pia anahusika na masuala ya Uchaguzi ( Election Officer) akiwapigia kura wagombea ambao wameomba kuwa wajumbe wa Tume ya Kimataifa ya Sheria. Nyuma anaonekana Mgombea wa Tanzania, Profesa Chris Maina Peter ambaye alishindana na wagombea wengine 13 kutoka Afrika ambapo walitakiwa nane kati ya hao 13. Afisa Lilian kwa nafasi yake kama Election Officer alikuwa na jukumu kubwa la kusaidia na kufanikisha mgombea wa Tanzania anapata kura za kutosha.

Na  Mwandishi Maalum,  New York

Profesa  Chris   Maina Peter ,  kutoka  Tanzania, ni kati ya     wagombea  nane miongoni  mwa wagombea   13 kutoka   Afrika, ambao jana  ( alhamisi )   Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa  liliwapiga kura  ya siri ya  kuwachagua kuwa  wajumbe wa   Tume ya Kimataifa  kuhusu masuala ya  Sheria ( International Law  Commission).

Ushindi wa Profesa  Maina ambaye ataitumikia   Tume   hiyo wa miaka mingine mitano  kuanzia Januari 2017, pamoja na juhudi   zake binafsi za kujinadi, kujitangaza, kwa wajumbe  193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Matifa, na  akisheheni sifa na  weledi mkubwa katika sheria za kimataifa. Ushindi  wake umechangiwa zaidi na   kazi kubwa iliyofanywa na   Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa  Balozi  Tuvako Manongi  kwa kushirikiana na Maafisa wake ambao walifanya kazi kubwa ya kumkampenia  na  kumwombea kura. 

 Ingawa Profesa Maina  anaingia kama  mtu binafsi  katika  kazi za   ILC anabeba   jina na kuipeperusha  bendera ya  Tanzania katika   Tume hiyo. Na kwa sababu hiyo,  ushiriki wa Serikali  katika kupendekeza jina lake pamoja na  kumsaidia katika kampeni ilikuwa ni sehemu  kubwa  ya  kufanikisha hatua hiyo muhimu ya kuendelea tena kuitumikia  Tume  kwa pindi cha pili cha miaka mitano.

 Katika  uchaguzi huo  wa jana ambao ulikuwa na ushindani mkubwa huku ukishuhudia  nchi kubwa kama  Ufaransa ikishindwa  kufurukuta.  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  lilitakiwa kuwachagua  wajumbe  34  watakaohudumu  katika  Tume hiyo kwa mgawanyo wa wajumbe   nane kutoka Afrika,    wajumbe  Saba kutoka  Asia-Pacific ,  wajumbe  wanne kutoka Ulaya ya Mashariki,  wajumbe saba kutoka  Amerika  ya  Kusini  na Visiwa vya  Caribbean  na  wajumbe  nane kutoka  nchi za Ulaya Magharibi na  nchi nyingine.

 Baada ya  upigaji  huo wa kura ya  sira,  washindi waliotangazwa   kwa   upande wa Afrika, waliochaguliwa   ni  Chris Maina Peter(Tanzania) Ahmed Laraba (Algeria), Tacouba Cissé (Ivory Coast), Dire D. Tladi (South Africa), Hussein A. Hassouna (Misri), S. Amos Wako (Kenya), Charles C. Jalloh (Sierra Leone) na Hassan Ouazzani Chahdi (Morocco).

 Kutoka  Asia-Pacific  waliochaguliwa ni  Ali bin Fetais Al-Marri (Qatar), Mahmoud Daifallah Hmoud (Jordan), Huikang Huang (China), Shinya Murase (Japan), Hong Thao Nguyen (Vietnam), Ki Gab Park (Jamhuri ya Korea ) na Aniruddha Rajput (India). 
Waliochaguliwa  kutoka  Amerika ya Kusini na Caribbean ni  Carlos Argüello Gómez (Nicaragua), Juan Manuel Gómez-Robledo (Mexico), Claudio Grossman Guiloff (Chile), Juan Jose Ruda Santolaria, (Peru), Gilberto Vergne Saboia (Brazil), Eduardo Valencia -Ospina (Colombia) na Marcelo Vázquez-Bermúdez (Ecuador).

Wajumbe kutoka Ulaya ya Mashariki waliochaguliwa ni   Bogdan Aurescu (Romania), Kirumi Anatolyevitch Kolodkin, (Shirikisho la Urusi), Ernest Petric (Slovenia) na Pavel Šturma (Jamhuri ya Czech).

Kwa upande wa  Ulaya Magharibi na  nchi nyingine  waliopita ni , Concepción Escobar Hernández (Hispania), Patrícia Galvão Teles (Portugal), Marja Lehto (Finland), Sean David Murphy (United States), Georg Nolte (Ujerumani), Nilufer Oral (Uturuki), Agosti Reinisch (Austria) na Michael Wood (United Kingdom).

Majukumu   ya  Tume ya  Kimataifa kuhusu  sheria   pamoja  na mambo mengine, ni  kukuza na kuendeleza sheria za kimataifa,  kutoa ushauri wa kitafiti kuhusu sheria mbalimbali, kupitia  masuala yahusuyo  sheria na  mikataba ya kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...