Na Humphrey Shao, 
Globu ya Jamii. 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. 
Rais Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko. 
 “Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” Amesema Rais Magufuli. 
 Amemtaka pia kuendelea kupiga kazi na kumwabia kuwa yeye yupo nyuma yake kwani amevunja mwiko wa viongozi waliokuwa wanapendelea kukaa ndani. Kwa upande wake mkuu huyo wa mkoa aliendelea kuwa mtiifu huku akimsikiliza Rais Magufuli kwa Makini juu ya pongezi anazopewa mbele ya watu kwani ameweza kurudisha imani kwa viongozi wa serikali ambayo iliondoka kwa watu kutokana na ujinga wa watu wa chache. Mhe. Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...