RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.

Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika  maisha yao. 

"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele  yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...