Na  Mwandishi Maalum, New  York
Rais wa  Mahakama ya   Kimataifa ya  Makosa ya Jinai ( ICC) Jaji Slivia Fernandez de  Gumendi,  jana  (Ijumaa),  amekutana na kufanya  mazungumzo na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Matiafa,  Balozi Tuvako Manongi
Katika  Mazungumzo  hayo baina ya   Jaji  Gumendi na  Balozi  Manongi  yaliyofanyika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania,   Rais wa ICC aliishukuru Tanzania kwa hotuba yake   iliyotolewa na Balozi  siku ya Jumatatu wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  lilipopokea na  kujadilia Ripoti ya  ICC.
Kwa  mujibu wa  Rais wa ICC Jaji Slivia Fernandez  de Gumendi  hotuba  ya    hiyo ya  Tanzania  ilikuwa   yenye uwiano (balanced)  na pia  ilitoa  ushauri au mapendekezo ya namna gani  Mahakama hiyo  inavyoweza kuboresha uhusiano  na  wanachama wake  kwa mujibu wa Mkataba wa Roma.
“  Nilikusikiliza  kwa makini sana  wakati  ulipokuwa unatoa hotuba  yako,   nilinukuu  kila  hoja   ulizokuwa unazizungumza . Hotuba   ya  Tanzania ilikuwa yenye  uwiano    (balanced) na ningependa  kuitumia   fursa hii kuishukuru   Tanzania kwa hilo.
Rais   huyo wa ICC amekiri kwamba anadhani ni wakati  muafaka  kwa wadau wa pande  mbili  kukaa na kuzungumza  kama ambayo  Tanzania  na wanachama  wengine wameshauri hasa kutokana na kile  alichosema, kwamba, kila nchi imekuwa na  tafsri  tofauti  na  uelewa tofauti  kuhusu baadhi  ya  vipengere  (articles) zinazohusu Mkataba wa Roma  unaounda  Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Kwa upande wake Balozi Manongi amesema,   ushauri na mapendekezo ambayo  yametolewa  na Tanzania pamoja na nchi nyingine hayalengi katika  kutaka  kubadili  Mkataba  wa Roma  au kuipunguzia  nguvu ya  kiutendaji  Mahakama hiyo.
“Tungependa sana  ieleweke kwamba tunaposhauri kukaa na kuzugumza  kusitafsiriwe kana kwamba tunataka kupunguza nguvu ya utendaji wa  chombo hiki ambacho  wote tunaamini kwamba  kinastahili kuwapo. Tunashosema na kusisitiza, kwamba   kila  upande unahoja  za msingi basi tuzijadili kwa kuzungumza” akasisitiza  Balozi  Manongi.
Rais wa  ICC na  Balozi Manongi  walibadilishana mawazo juu  na masuala mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya  ICC ikiwa ni pamoja na  kuangalia ni maeneo gani ambayo   Mahakama na wanachama  wake  wanaweza kujadiliana . 
  Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi akiwa  katika  mazungumzo  na  Rais  wa Mahakama ya   Kimataifa ya Makosa ya Jinai  ( ICC)  Jaji  Slivia Fernandez de Gumendi. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika  Ubalozi wa Tanzania,  Rais wa ICC alitumia fursa hiyo  kutoa shukrani zake kwa Tanzania  kwa   hotuba   ambayo si tu ilikuwa na  ushauri wa namna ya  kuimarisha  ushirikiano baina ya  Mahakama hiyo na  Wanachama wa Mkataba wa Roma  hususani kutoka nchi za Afrika lakini  pia kwamba ilikuwa ni  hotuba ya    uwiano.  Jumatatu  wiki hii Tanzania ilikuwa kati ya nchi zilizozungumza wakati  Ripoti ya utendaji kazi  ya ICC ilipowasilishwa katika Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa. 
Balozi  Tuvako Manongi na Rais wa ICC Jaji Gumendi  mara baada ya kumaliza  mazungumzo yao ambayo  yaligusia  masuala mbalimbali  kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya  Makosa ya Jinai ( ICC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...