Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kupitia upya taratibu na kanuni zilitumika kwenye umiliki wa shamba la Manyara Ranch lililopo tarafa ya Makuyuni.

Alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja katika tarafa hiyo nakutembelea shamba la Manyara Ranch ambalo wananchi wanadi ni mali yao baada ya umiliki wake kufutwa mwaka 1999 nakurudishwa kwa wananchi.

Hata hivyo bado kuligubikwa na maswali mengi ya hati miliki ya shamba kuandikwa jina la Tanzania Land Conversation Trust (TLCT)  ambacho ni chombo cha kusimamia shamba hilo na badala ya mmiliki mkuu ambae ni Halmshauri ya Wilaya ya Monduli, hali iliyopelekea Gambo kutolea maamuzi ya hati miliki iandikwe Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.

“Naiagiza Halmashauri kuhakikisha hati miliki ya shamba hili isomeke jina la Halmashauri badala ya TLCT kwasababu tayari shamba lilisharudishwa kwa wananchi na halmashauri ndio msimamizi wa mali za wananchi”,alisema.
Akisoma taarifa fupi ya shamba la Manyara Ranch Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya African Wildlife Foundatio(AWF)ambao ndio wanaendesha shughuli zote katika shamba hilo bwana Fidelisi Ole Kashe amesema taasisi hiyo iliingia mkataba wakuendesha shughuli zote ndani ya shamba kutoka kwa TLCT baada ya chombo hicho kushindwa kuziendesha.

Aidha akifafanua zaidi Mkurugenzi mtendaji wa TLCT bwana Boniface Ngimojiro alisema TLCT iliundwa na bodi ya halmashauri ya wilaya ya Monduli ili isimamie na kuendesha shughuli zote za shamba la Manyara Ranch na baada yakushindwa kuendesha ndipo wakazikabidhi kwa AWF.

Hata hivyo Gambo alisema ataunda timu yakuchunguza shughuli zote za TLCT kwa mda wa miaka 10 ya nyuma ilikusaidia kufahamu zaidi kama chombo hicho bado kinahitajika katika uwendeshaji na usimamizi wa shughuli za shamba la Manyara Ranch.
Gambo amekuwa akifanya ziara zake katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa lengo lakusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe Mrisho Mashaka Gambo akihutubia wananchi wa kijiji cha Esilalei katika tarafa ya Makuyuni Wilayani Monduli.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Wildlife Foundation akisoma taarifa fupi ya mradi wa shamba la Manyara Ranch kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(hayupo pichani),pembeni yake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifuatilia taarifa hiyo.

 Wananchi wa kijiji cha Esilalei wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Makuyuni alipofanya ziara katika tarafa hiyo iliyopo Wilayani Monduli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...