Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amemuagiza Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni Meya Mteule wa Manispaa hiyo Boniphace Jacob kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano katika shule  mpya ya Sekondari Urafiki.
Mhe. Makonda ameyasema hayo wakati akizindua shule hiyo ya urafiki ikiwa ni moja ya muendelezo wa ziara yake ya siku 10 ya Mkoa wa Dar es Salaam. Amesema viongozi wa kisiasa inabidi waache siasa za ujanja ujanja na badala yake kuwatumikia wananchi.
"Diwani wa hapa anavtakribani miaka mitano hivyo inabidi apambane na kuhakikisha uhaba wa vyumba hivyo vitano unakamilika".
katika hatua nyingine RC Makonda amewataka wanafunzi kujitahidi kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuingia katika soko la ushindani wa ajira kwa vitu vingi vimetawaliwa na Sayansi.
Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea pia barabara ya Ubungo River Side na kuwataka wananchi wajitolee maeneo yao ili kupisha ujenzi wa barabara ambao ulikuwa ni changamoto kwao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akikata utepe wakati wa kuzindua shule ya Sekondari ya Urafiki  jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka jiwe la Msingi katika shule ya Sekondari Urafiki leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akigangua kiwanda  cha Paper craft  cha Tanzania Tooku kilichopo  Mabibo Extenal leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akikagua ujenzi wa barabara ya ilipo katika Mtaa wa Kibangu  Kata ya  Makuburi unaoanzia Riverside mpaka kanisa la Mzee wa Upako ambapo pia alisikiliza kero za wananchi  waliopisha upanuaji wa Barabara leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...