Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wakazi wa Mkoa huo ambao taka zimezagaa eneo la mitaa yao na hazijafuatwa kubebwa wazipeleke nje ya ofisi ya Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti atafanya utaratibu wa kuzisafirisha.
" Katika mkoa wangu wa Dar es Salaam sitaki nisikie mazingira yenu machafu kila Mtaa nahitaji uwe  msafi. Safisha mazingira yenu  mlipie taka ushuru kila mwezi na taka zikitekelezwa bila kuzolewa na Wakandarasi pelekeni ofisi ya Mwenyekiti wenu." alisema Makonda. 
Alisema ifike wakati watu wabadilike ili  kutunza mazingira yetu  kila mmoja   kufanya usafi ni wajibu wake.
"Nahitaji mji wa Dar es saalam ubadilike nataka kuona usafi  tuepuke mazingira machafu lengo likiwa ni kupambana na mgonjwa ya milipuko,"alisema.
Katika ziara yake Makonda  pia alitembelea eneo la Kawe ambapo alitembela nyumba zilizojengwa katika maeneo hatarishi ambapo alitoa agizo kwa TANESCO na DAWASCO kuondoa miundombinu iliyopo katika eneo hilo ili wananchi waondoke katika eneo hilo.
Makonda alisema eneo hilo sio salama kwa makazi ya watu hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kuondoka.
 Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa Kikundi cha wa Mama wanaohudumia mzunguko wa Kigogo Elizabeth Matarimo  jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  akipokea pipa la kuwekea takataka kutoka kwa  Msemaji wa Kiwanda cha Nondo MM Steel,Abuu Mlawa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kigogo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, alitembelea eneo la Kawe ambapo alitembela nyumba zilzojengwa katika maeneo hatarishi na kutoa agizo kwa TANESCO na DAWASCO kutoa miundombinu iliyopo katika eneo hilo leo jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...