Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa mkuu wa wilaya ya Kigamboni
Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wananachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika."Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya watumishi umma hawafanyi kazi, ni wapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara," alisema Mkonda.
Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali inawafanya kazi kuanzia ngazi ya vitongoji.Aidha mkuu huyo alitembelea pia mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo alishuhuda uharibifu mkubwa wa mazingira na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi kuwashghulikia wote watakaoendelea kuchimba kokoto eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizindua mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.   Katika ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na kulia ni Mkurungenzi wa manispaa ya Kigamboni,Stepheni Katembe.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza machache katika   uzindunzi wa mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na Kamisha wa Polisi Simon Sirro, wakimuangalia mmoja wa vijana wa kituo cha kuwasaidia vijana waliothirika na dawa za kulevya cha PEDEREF Sober,Kigamboni  ambaye alikuwa akitia ushahidi wa jinsi alivyoathiriwa na dawa hizo kwa kubeba dawa tumboni, wakati wa ziara ya mkuu huyo wa mkoa, wilayani humo,leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua uharibifu wa mazingira machimbo ya kokoto Mjimwema jijini Dar  es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua machimbo ya kokoto yalipo Mjimwema jijini Dar  es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vijana wa Sober House  iliyopo  Vijibweni leo jijini Dar es Salaam.
 amanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro  akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zinazo jitolea  kusikiliza  changamoto na kero za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ONGOZA KUTOKEA NYUMA NA KUWAFANYA WENGINE WAAMINI WAO NDIYO WAKO MBELE,MKUU MAKONDA KAZI NZURI UNAFANYA, LAKINI NAKUOMBA SANA PUNGUZA MANENO, TUMIA SANA BUSARA, USINGOMBANE NA WATU WALIO KARIBUI NA WEWE PLEASE, SWALA LA RUSHWA SIO NZURI, JE KINANANI WALIO TAKA KUKUPA PESA MBONA UKUWATAJA MBELE YA WAZIRI MKUU? LAKINI ILIKUWA VYEPESI KWAKO KUMTAJA KAMANDA WAKO WA DAR NA WENGINE SIO VIZURI,

    DR, JAMESSY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...