THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC SHINYANGA AKAGUA NYUMBA ZA WATUMISHI AFYA WILAYANI KISHAPU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.  Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu na kukagua mradi wa nyumba za watumishi wa Idara ya Afya zilizojengwa kwa msaada wa Mfuko wa Benjamin William Mkapa.
Katika ziara hiyo Mhe. Telack akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alitembelea nyumba hizo katika kata za Shagihilu, Mwakipoya na Idukilo ambazo tayari zimekamilika kwa ajili ya makazi.
Mkuu huyo wa mkoa aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazoikabili miradi hiyo na sekta ya afya kwa ujumla zitatuliwe ziwe zimetatuliwa.
Aliitaka Idara ya Afya kushirikisha Idara ya Ujenzi katika kutekeleza miradi inayohusu ujenzi wa mindombinu mbalimbali katika sekta hiyo muhimu kwa kuwa ndiyo wataalamu.
Awali wakati akisoma taarifa ya halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga alisema jumla ya zahanati 22 zinajengwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau.
Magoiga aliongeza kwa kusema kuwa kukamilika kwa zahanati hizo katika kata mbalimbali kutasaidia kutatua changamoto ya vifo vya wajawazito na watoto.
Alibainisha kuwa hivi sasa halmashauri ina magari ya wagonjwa (ambulance) manne ambapo matatu kati yake yalitolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNFPA) wakati moja lilinuliwa na halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (mbele) akikagua moja ya nyumba za watumishi wa Afya kata ya Shagihilu zilizojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Benjamin William Mkapa. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa, Mwita Ngutunyi (mwenye suti).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji mara baada ya kuwasili katika nyumba ya mtumishi wa Zahanati ya Kata ya Idukilo wakati wa ziara yake wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa akifungua mlango wa moja ya nyumba kujionea mradi huo uliofadhiliwa na Mfuko wa Benjamin William Mkapa wakati wa ziara yake.
Mkuu wa Mkoa akiwasili katika zahanati ya Badi iliyopo Kata ya Mwakipoya wilayani Kishapu kukagua miradi ya nyumba za watumishi wa Afya. Wengine pichani kuanzia kushoto Afisa Mipango Wilaya, Mang’era Mang’era, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya, Stephen Magoiga (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa, Mwita Ngutunyi (mwenye suti).
Ukaguzi wa nyumba unaendelea huku Mhandisi Ujenzi Wilaya, Samson Pamphil (kushoto) akichukua taarifa muhimu.