Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo  na moja wa vijana wa Skauti eneo la Visakazi alipotembelea jimboni humo.

Mwenyekiti wa Chama cha CCM Tawi la Visakazi akieleza baadhi ya malalamiko ya wananchi mbele ya  Mbunge wao Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye ofisi ya chama hicho katika mkutano.


Mbunge Ridhiwani Kikwete wa pili upande kushoto  ashiriki katika mazishi  Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo na wa kwanza upande wa kulia ni Sheikh Hussein wa Bwilingu akitoa neno la Mawaidha katika msiba
-------
Wananchi katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, wamekiri kuona mwanga kwa jinsi viongozi wanavyotatua matatizo yao, kufuatia kuongezeka kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa kero zao mbele za viongozi na kujadiliana utatuzi wake kwa pamoja.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya wananchi wa kitongoji cha Visakazi kata ya Ubena Chalinze na Mbunge wa Chalinze RIDHIWANI KIKWETE, ambapo sehemu kubwa ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kukubali kwamba mikutano ya majadiliano mara kwa mara kati ya viongozi na wananchi huongeza ufanisi katika utendaji. 

Naye Mbunge wa Chalinze kwa upande wake amebainisha kuwa mikutano hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kiuongozi ambao amejiwekea katika kuhakikisha anatatua kero za wananchi wake kwa wakati muafaka na kwa kiwango kinachotakiwa.

Wakati wa mkutano huo, wananchi hao wameshukuru kwa kazi kubwa ambazo tayari zimefanyika katika jimbo hilo ikiwemo uimarishaji wa huduma za  afya, elimu na pamoja na mambo mengine ya kijamii.

“Mbunge huyu amekuja na staili kama ya wakati wa mzee wake wananchi tunapewa nafasi tunasema hata yetu binafsi naamini hii itasaidia sana na utakuwa karibu na wananchi wako", alisema Bi Semeni Masound, 

Aidha  wameelezea kuridhishwa na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

katika hatua nyingine Mbunge Ridhiwani ameshiriki katika mazishi ya Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo.

Mbunge huyo ataendelea na ziara ya kutembelea wananchi tarehe 5 novemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...