Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Henry Shekifu kufuatia kifo cha Balozi mstaafu Mhe Waziri Juma, kilichotokea juzi tarehe 22 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Mhe Waziri Juma ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa muda mrefu, Katibu wa CCM ngazi ya Mkoa, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), pia amekuwa msimamizi wa ujenzi wa reli ya TAZARA, Mkuu wa Mkoa, na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali.

Mhe. Waziri, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania na kuleta maendeleo hapa nchini utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.
Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 
Imetolewa na:- 
                   
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
24.11.2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...