THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERENGETI BOYS WAKWAA PIPA KUELEKEA KOREA YA KUSINI

Na Dac Popo wa Globu ya jamii
Kikosi cha wachezaji 19 wa timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 wameondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo. 
Akizungumza baada ya kuwaaga wachezaji hao katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere afisa habari wa shirikisho la kabumbu Tanzania TFF Alfred Lucas alisema kuwa mashindano hayo yanayojumuisha mataifa manne yameandaliwa na shirikisho la kandanda la Korea ya Kusini na kupewa baraka na FIFA. 
Amesema kuwa hiyo ni nafasi nzuri ya mazoezi kwa timu hiyo kwani iwapo rufaa iliyokatwa na TFF kuhusu timu ya taifa ya Congo ya umri huo kumchezesha mchezaji aliyezidi umri timu hizo zilipopambana kuwania kushiriki mashindano ya Afrika itafaulu basi timu yetu itakuwa imepata mafunzo ya kutosha na kujiweka vizuri zaidi kwa fainali hizo zitakazofanyika Madagascar. 
Wakati huo huo Alfred Lucas amesema kuwa timu yoyote iliyo katika Ligi Kuu ya kandanda nchini VPL ambayo haitapeleka timu yake ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 katika mashindano yake yatakayofanyika katika vituo vya Kagera na Dar es salaam itakumbwa na adhabu ya faini na kunyang’anywa pointi. 
Ametanabaisha kuwa kutokana na kanuni ya 42 kifungu cha 27 ya kanuni za ligi timu ikikosa mchezo wa kwanza itapokwa pointi 3 na faini ya sh.2,000,000/ na kama haitapeleka timu basi timu yake kubwa itapokwa pointi 12 kutoka katika pointi ilizonazo kwenye msimamo wa ligi ulivyo sasa. Ametoa kauli hiyo kufuatia klabu za Yanga na African Lion kutishia kutopeleka timu zao za vijana katika kituo cha Kagera ambazo wamepangiwa,mashindano hayo yamepangwa kuanza tarehe 16 ya mwezi huu.
 Afisa Habari wa Shirikisho la Kabumbu Tanzania TFF Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari juu ya  timu ya vijana  walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 kuondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.
Serengeti Boys wakiwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.
Vijana  wa Serengeti Boys wakiingia kwenye eneo la ukaguzi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.