Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (katikati) akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha
kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika inayoratibiwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa wadau wa
utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Mtaalam wa
Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi anayefuatia ni Mtaalam wa
Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya na wakwanza kulia ni
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bibi. Deirdre Solani.
Na Genofeva Matemu
Serikali imeahidi kuhifadhi kumbukumbu na takwimu sahihi za urithi wa
Utamaduni usioshikika kwa lengo la kuuendeleza na kuiwezesha jamii
kuulinda kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua warsha ya siku
kumi iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika leo Jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo Prof. Gabriel amewataka washiriki
kujifunza vizuri ili baadaye waweze kusaidia katika kuwekeza, kuibua,
kutambua na kutunza urithi wa utamaduni ushioshikika kwani hiyo ndio
njia mojawapo itakayowavutia watalii wengi kuja nchini kujifunza
tamaduni zetu zisizoshikika.
Mtaalam wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa wadau wa utamaduni iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mtaalam wa Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi.
“Utamaduni ni nta inayowaweka watu pamoja, ni vyema mafunzo haya na
utaalamu mtakayoipata izingatie kuibua fursa na kutambua tamaduni
ambazo hazishikiki kwani serikali ina malengo na matumaini makubwa
sana kutoka kwenu” alisema Prof. Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lily Beleko amesema kuwa
Tanzania iliweka saini na kuridhia mkataba wa kulinda urithi wa
utamaduni usioshikika ambao ulipitishwa na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzanzaia mnamo mwaka 2011.
Anaongeza kuwa baadaye UNESCO kwa kushirikiana na Wizara
inayohusika na mambo ya Utamaduni wamekua wakishirikiana katika
kutoa mafunzo kwa wadau wa utamaduni na watu binafsi kuhusu namna
ya kuhifadhi urithi wa utamaduni usishikika ambapo mafunzo hayo
yanafanyika kwa mara ya nne sasa huku lengo likiwa ni kutekeleza
mkataba huo.
Aidha Bibi. Beleko amesema kuwa watanzania wengi wamekua wakidhani
kuwa utamaduni ushioshikika unahusiana na mambo ya kichawi hivyo
kutotilia maanani umuhimu wake kitu ambacho si kweli kabisa kwa kuwa
maana halisi ya utamaduni usioshikika unahusisha vitu vinavyohusiana na
mazingira, maendeleo ya watu pamoja na mila na desturi zao yakiwemo
maongezi, nyimbo, maigizo, midundo ndani ya ngoma ambayo
yanaambatana na ala.
Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bw. Mathias Luhanya amesema kuwa dhumuni la
warsha ni pamoja na kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni namna ya
kuhifadhi urithi wa utamaduni usioshikika ili baadaye waweze
kuorodhesha urithi huo kwani Tanzania ina bahati ya kuwa na jamii zaidi
ya 120 hivyo ni matarajio kuwa urithi wa utamaduni usioshikika
umesheheni ndani ya kila jamii.
Wadau wa Utamaduni wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni usioshikika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...