Na Anthony John wa Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) Bw.Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali imeanza Ujenzi wa reli ya kati,ujenzi wa kiwango cha Standard Gauge yenye upana wa Mita 1.345.

Akizungumza Jijini Dar es salaam na Waandishi wa Habari,Kadogosa amesema kuwa ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kwanza katika nchi ya Tanzania hasa baada ya baada ya Uhuru utapelekea kuleta na kuhamasisha maendeleo kwa haraka katika sekta ya Kilimo,biashara,Madini na viwanda.

Hata Hivyo Mkurugenzi huyo amesema kukamilika kwa mradi wa Reli ya kati utaleta manufaa mengi ya kiuchumi na ya kijamii na kusaidia kuboresha pamoja na kuunganisha usafirishaji kwa nchi zisizokuwa na bandari kuelekea masoko ya Afrika na Dunia kwa ujumla.

"Kukamilika kwa Reli ya kati Utavutia uwekezaji katika maeneo ambayo mfumo huo wa Reli utapita na utaboresha usafirishaji,lakini pia utachochea maendeleo ya shughuli za Madini na usafirishaji wa nidhaa nje ya nchi, utasaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza gharama kubwa ya ukarabati wa barabara,"amesema Kadogosa.

Pia ameongeza kuwa miradi hii imekuwa ikigharamiwa na Serikali ilikutimiza azma yake kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa ajili ya jamii ya w atanzania hasa tunapoelekea katika uchumi wa viwanda kupitia sekta ya usafirishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzani TRL akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na ujenzi wa mradi wa reli ya reli ya kati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...