THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERIKALI YAJIPANGA KUKUZA UCHUMI WA WAKAZI WA BUSOKELO

Serikali imesema itaijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Katumba-Mbambo hadi Tukuyu KM 79.4 ili kuiunganisha kwa lami wilaya mpya ya Busekelo na Wilaya nyingine za mkoa wa Mbeya na hivyo kukuza uchumi wa wilaya hiyo. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo unaendelea katika sehemu ya Lupaso hadi Bujesi KM 10 na kumtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kampuni ya Chongqing International Construction Corporation (CICO) kuongeza kasi ya ujenzi huo kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kwenye mkataba.

“Nawaomba wananchi wa Busokelo msimcheleweshe mkandarasi kufanya kazi yake kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuchelewesha ujenzi wa barabara hii kwa kufungua kesi za kudai fidia kwani kwa kufanya hivyo kunachelewesha maaendeleo ya ujenzi wa barabara hii”. amesema Eng. Ngonyani.

Eng. Ngonyani amewataka wananchi wa Wilaya ya Busokelo kushirikina na viongozi wao na kutoa ushirikiano unaostahili ili kasi ya ujenzi wa baraba za lami katika maeneo yao isikwamishwe na wananchi wachache.

Akiwa wilayani Busekelo Naibu Waziri huyo amekagua barabara za Kata ya Mpata na Luteba ambazo zinasimamiwa na halmashauri na kuahaidi kushirikiana na Wizara nyingine ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo inayozalisha mazao mengi chakula na biashara yanayosafirishwa katika miji mikubwa nchini. 


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wakazi wa kata ya Mpata wakati alipokagua miundombinu ya barabara katika kata hiyo. 
Wakazi wa mwakaleli wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo pichani). 
Mbunge wa Busokelo Mhe. Atupele Mwakibete akiongea na wananchi wa jimbo lake wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea kukagua miundombinu ya barabara jimboni humo. 


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Mpata wilayani Busokelo mkoani Mbeya ambao wapo tayari kutoa maeneo yao ili kupisha ujenzi wa barabara inayounganisha kata hiyo na eneo la Mwakaleli.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA