Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.

WIZARA ya ardhi , nyumba na Maendeleo ya makazi nchini imetolea ufafanuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na Wananchi juu ya ulipaji wa fidia za mali zao mara baada ya kuondolewa kwenye maeneo yao na kupelekwa kwenye maeneo mengine.

Akuzungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mthamini Mkuu wa Serikali Bi. Evelyne Mugasha ameeleza kuwa malalamiko hayo ya fidia hutokana na sababu kadhaa ikiwemo  viwango vinavyotumika kutatmini ardhi vinatakiwa viendane na soko, lakini wakati mwingine  hata kama viwango vya soko vimetumika bado  baadhi ya wananchi hudai viwango vya juu kuliko uhalisia wa ubora wa maendeleo yao.

“Zoezi la fidia lipo wazi na ni muhimu wananchi waelewe, Sheria inasema wananchi waondolewe na wapelekwe sehemu ambayo inalingana na hali aliyokuwa nayo awali, tofauti na wanachi wanavyofikiria ili iwe haki kwa mwananchi na mtoa fidia”.

 Bi. Mugasha ameeleza kuwa fidia hupaswa kulipwa au kutolewa ndani ya miezi sita tu na iwapo itachelewa zaidi watoaji fidia watalazimika kutoa riba ya fidia hiyo,pia fidia hulipwa kutokana na wakati uliopo na si wakati ujao kutokana na kifungu cha sheria na 3 (1) (g)cha sheria z ardhi na 4 na sheria ya ardhi ya vijiji na 5 za mwaka 1967.

Naye Mthamini Mwandamizi Bwana. Juma S. Jingu ameeleza juu ya changamoto wanazokutananazo, moja ya changamoto kuu ni kutokuwepo kwa uelewa wa ujazaji fomu Na.70 ambayo madhumuni yake ni kumtaka mwananchi kutoa maelezo  kadhaa kuhusu mali yake ili iweze kufidiwa kihalali, pia ukosefu wa elimu juu ya uthamini na fidia Pamoja Ucheleweshaji wa ulipaji vidia.

Bwana Jingu ameongea kuwa kutokanan na changamoto hizo ni vyema mwanachi wakapewa elimu ya utambuzi juu ya suala hili ili waweze kuelewa kwa undani juu ya uthamini na ulipaji fidia wa mali zao na kujua sheria zilizowekwa kwa manufaa yao ili kuepuka malalamiko na changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...