Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MASHINDANO ya kuchezea mpira  (Football Freestyle)  yaliyoandaliwa na chama cha mchezo huo Freestyle Football Tanzania (FFT) yanatarajiwa kuanza Novemba 19 kwa Wilaya tatu za Jiji la Dar es Salaam Temeke, Ilala na Kinondoni na  uzinduzi wa shindano hilo unatarajiwa kuanzia kwenye viwanja vya Mwembe Yanga.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo unayodhaminiwa na kinywaji cha Red bull ikishirikiana na Clouds TV kupitia kipindi cha Sports Bar anatarajiwa kuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.

Akizungumza na Mratibu wa shindano hilo Jacob Mbuya amesema kuwa washiriki  wa shindano hilo watajiandikisha bure  na washiriki wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 15 na kuendelea huku fomu za ushiriki zinapatikana Clouds TV na Ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni pamoja na mitandao ya kijamii kupitia kurasa zao.

Mashindano yanatarajiwa kuanzia Wilaya ya Temeke Novemba 19 na kutapatikana washiriki watano na baadae kuhamia kwenue wilaya   ya Ilala ambayo pia itatoa washiriki watano  huku Kinondoni ikitoa sita ambao wataingia Fainali itakayochezwa Coco Beach, Disemba 11 na kwa upande wa  Wilaya ya Ilala shindano hilo litafanuyika kwenye viwanja vya Boma, Novemba 26 kabla ya kuelekea Kinondoni kwenye uwanja wa Tp Sweet Corner, Disemba 3. Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT)  Pascal Chang'a amesema kuwa wameamua kuanza kufanya mashindano haya na kupata vipaji ambao watawapa fursa ya kwenda kimataifa zaidi kwani huwezi kwenda kushiriki kama hujafanya nchi kwako na alitaja baadhi ya sheria za mchezo huo kuwa ni kila mshiriki atapewa sekunde 30 za kuchezea mpira, mchezaji atakuwa peke yake jukwaani na pia akidondosha mpira atakuwa amepoteza pointi.
Naye Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy amesema kwua wameamua kushirikiana na FFT ili kuweza kuibua vipaji vya vijana katika mchezo huu na pia wao wamedhamini kwa kila kitakachokuwa kinahitajika.
Katibu wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey akizungumza na waandishi wa habari wakati kuhusiana na mashndano ya kuchezea mpira yanayotarajiwa kuanza Novemba 19, kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na kulia ni Mratibu wa Shindano hilo Jacob Mbuya.
Mratibu wa Shindano la kuchezea mpira Freestyle Football Jacob Mbuya akizungumza na waandishi wa habari na kutoa utaratibu wa ushiriki kwa vijana kuanzia miaka 15 na kuendelea kulia ni 
Katibu wa  Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy  na mwisho ni Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT)  Pascal Chang'a. Picha na Zainab Nyamka.





















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...