THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Lindi Geodfrey  Zambi ameahidi kuunda kamati kwa ajili ya ufuatiliaji wa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kata ya Somanga wilayani Kilwa. https://youtu.be/P169k8eiyj0

SIMU.TV: Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira ametoa agizo kwa wataalamu kupima maji yanayotoka katika mgodi wa Geita ili kubaini kama ni salama kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo. https://youtu.be/wTqufjWeyIE

SIMU.TV: Mkamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali inashughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda ili kuboresha sekta hiyo. https://youtu.be/KXaZ3AH3FVM

SIMU.TV: Wakala wa usajili wa biashara na leseni BRELA umewataka vijana nchini kuchangamkia fursa ya mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kupata maarifa ya kujiajiri. https://youtu.be/N3s_8aOWE04

SIMU.TV: Askari sita wa kikosi cha usalama barabani kutoka mikoa mbalimbali nchini wameondolewa katika kikosi hicho na watapangiwa kazi nyingine kutokana na kutotekeleza majukumu yao kikamilifu. https://youtu.be/6R9dT-bOdfw

SIMU.TV: Rais Dr. John Pombe Magufuli amekipongeza chuo kikuu huria kwa kutoa elimu ya juu kwa watanzania wengi na kuahidi serikali itaunga mkono kwa kuboresha miundombinu ya elimu. https://youtu.be/JsoEI_kTYDY

SIMU.TV: Tanzania imeshauria kutumia fursa za kijiografia zinazoizunguka ili kuweza kufika malengo ya uchumi wa viwanda. https://youtu.be/bmfzcncKHMU

SIMU.TV: Viongozi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kuitafsiri sera ya uwezeshaji wananchi kwa vitendo ili kuwafanya wananchi kuwa na mabadiliko ya kifikra katika uzalishaji. https://youtu.be/wQ6fxBOzQmQ

SIMU.TV: Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo imesema Tanzania itaendeleza ushirikianao wa sanaa uliopo kati yake na nchi ya China. https://youtu.be/Iv_-ZnuHwRY

SIMU.TV: Miss Tanzania wa mwaka 2016 Diana Edward amekabidhiwa bendera kwa ajili ya kuelekea nchini Marekani kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia. https://youtu.be/Uv0H-6uPS8o

SIMU.TV: Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu ambapo atakua nje kwa muda wa miezi minne. https://youtu.be/BFbyy-mscM4