Na Dac Popo wa Globu ya Jamii
 Katika harakati za Taasisi zisizo za kiserekali za kusaidia vijana kuweza kupata elimu ili kujenga maisha yao ya baadaye, taasisi ijulikanayo kwa jina la Darwin imesaidia vijana wapatao 50 kupata nafasi katika  vyuo vya juu nje ya nchi.
 Taasisi hiyo iliyoanzishwa miezi 6 iliyopita imefanikisha kuwapatia vijana hao kupata elimu hiyo katika nchi za China, India, Malaysia, Canada na Australia. 
 Akieleza hayo katika hafla fupi ya kuwaaga baadhi ya vijana hayo kwenye uwaja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Makungu J. Malando amesema taasisi yake ambayo inatambuliwa na T.C.U.  na inasaidia vijana kupata visa, malazi, usafiri na scholarship. 
 Naye mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake amebahatika kupata nafasi hiyo Bw. Hamis Suleimani ameishukuru Darwin kwa kufanikisha safari hiyo kwa kijana wake na kusisitiza kuwa taasisi hiyo inaangalia zaidi ubora wa vyuo wanavyo watafutia nafasi vijana wa Tanzania.
 Mkurugenzi wa taasisi ya Darwin Bw. Makungu Joseph Malando akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
 Mzee Hamis Suleiman ambaye ni mzazi wa mmoja wa vijana wanaokwenda kusoma katika moja ya vyuo vikuu nje ya nchi akiongea katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Darwin Bw. Makungu Joseph Malando akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na baadhi ya vijana wanaokwenda masomoni nje ya nchi katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.picha  na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...