THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KAMBI MAALUM YA UPASUAJI YA WAGONJWA WA MOYO

Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Shalau akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tatizo la ugonjwa wa moyo kwa watoto katika mkutano wa waandishi wa Habari . Kulia ni  Russell Lee kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia.
  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kumalizika kwa  kambi maalum ya  siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo iliyofanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia. Kulia ni Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Dk. Godwin Shalau akifuatiwa na Russell Lee kutoka OHI. 
 Dkt. Jayme Bennetts ambaye ni bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo iliyomalizika jana ambapo wagonjwa waliofanyiwa upasuaji ni 17 kati ya hao watoto ni 12 na watu wazima ni watano. Kushoto ni Bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt. Peter Kisenge, akifuatiwa na Dkt. Benjamin Bierbach ambaye ni bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto,  na kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Bashir Nyangasa.
Picha na Anna Nkinda – JKCI