Unapowadia mwisho wa mwaka wizi
kupitia mtandao umekua ukishika kasi zaidi. Mataifa mengi duniani yamekuwa
yakikumbwa na wimbi kubwa la uhalifu mtandao unaoambatana na upoteaji wa pesa.
Itakumbukwa mwaka jana kuelekea mwisho wa mwaka ndio kirusi kipya aina ya
ModPOS kilionekana kwa mara ya kwanza na kilifanikiwa kudhuru maeneo mengi na
kusababisha kiasi kikubwa cha fedha kupotelea mikononi mwa wahalifu.
Mwezi huu wa Novemba pekee tayari kumekua na matukio mengi yenye
mlengo wa kuwapatia pesa wahalifu mtandao. Kwa sasa Uhalifu mtandao kpitia
kirusi cha RANSOMWARE kinachoendelea kushikakasi wamefanikiwa kupata mamilioni ya fedha.
Kirusi hiki kinapelekea mhalifu mtandao kumfungia uwezo mmiliki halali kutumia
kifaa chake akimtaka alipe kiasi cha pesa ili kurudishiwa huduma. Uhalifu huu
umepiga hodi Barani Afrika na hadi sasa wengi wameendelea kuathirika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...