THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDUMkuu wa Wilaya ya Arusha ametoa angalizo kwa wananchi wote kuhusu tahadhari ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeripotiwa kuwepo katika Mikoa mbalimbali na maeneo ya jirani na Wilaya hii.

Akizungumza kwenye kikao maalumu na watendaji wa Kata, Maafisa Afya pamoja na wadau wa Afya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Alexander Mnyeti ameelezea hatua ambazo Serikali ya Wilaya imechukua hadi hivi sasa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa kuwa ni:

-         Kuandaa kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaojitokeza –ipo katika Kituo cha Afya Levolosi
-         Kuagiza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa
-         Kusambaza  mabango, vipeperushi na miongozo  katika vituo vua kutolea huduma za afya, Ofisi za Kata na mitaa pamoja na maeneo ya mikusanyiko
-         Kufanya kikao na wadau wote na kuunda timu ya usimamizi wa mlipuko wa kipindupindu.

Kupitia kikao hiki kwa kauli moja wajumbe walikubaliana hatua za kuchukua ili kupambana na mlipuko:
-         Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi  kwenye maeneo yote yenye uhaba wa maji
-         Kuchukua Sampuli za maji katika Kata za pembezoni
-         Kupiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa,vyakula barabarani na pombe za kienyeji
-         Kutembelea kaya na kukagua uwepo wa vyoo na matumizi yake
-         Kugawa vidonge vya Kutibu maji kwenye kila  Kaya
-         Kuwachukulia hatua wote watakaokiuka wa kanuni za Afya

Pia wananchi walishauriwa kujikinga na ugonjwa huu kwa njia zifuatazo;
-         Kunywa maji yaliyochemchwa au yaliyowekewa dawa ya kuua vimelea
-         Kula chakula cha moto kilichotayarishwa katika hali ya Usafi.
-         Kunawa mikono kwa sabuni na maji ya kutitirika (usinawe ndani ya chombo).
-         Kuhakikisha matumizi bora ya choo na kinyesi cha watoto wadogo  kitupwe chooni
-         Kuepuka kula matunda bila kuyaosha na kunywa juisi na vyakula vinavyouzwa kiholela.
IMETOLEWA NA                            
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.

17  Novemba ,2016