THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Tanzania Kupata Bilioni 12 Za TradeMark East Africa Kusaidia Wafanyabiashara Wanawake

Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania (TWCC) jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Tanzania itafaidika na msaada wa Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania, zitakazotolewa na Taasisi ya TradMark, East Afrika, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika na kwa kuanzia, TradeMark,  itaanzisha madawati ya jinsia kwenye mipaka mitatu ya Holili, Kabanga na Mutukula. 
Ahadi ya fedha hizo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga (pichani), wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania, TWCC,  kujadili vikwazo kwa wafanyabiashara wanawake mipakani, uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Ulanga amesema  fedha hizo zitatolewa na TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade”  uliolenga kuwajengea uwezo kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa. 
Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12, kati ya hizo, Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kitapatiwa shilingi milioni 500. 
Akishukuru kwa msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bibi Jaquiline Mneney Maleko, ameishukuru TradeMark kwa msaada huo, na kuahidi utatumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. 
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
 TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji  wa  masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani. 
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia  ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina  matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com

Mwisho
 Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akifafanua jambo wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania  (TWCC)
Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania (TWCC)