Na: Geofrey Tengeneza

Tanzania jana iliwaongoza wananchi kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wageni na washiriki wa maonesho ya utalii ya World Travel Market (WTM) yanayofanyika jijini London nchini Uingereza kutoka mataifa kadhaa duniani kusheherekea siku ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika banda hilo huku watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakikaribishwa kuja kuzitembelea nchi za jumuiya hiyo na kujionea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda huu wa Afrika.

Sherehe hiyo iliyohudhuriwa pia na mawaziri, mabalozi, maafisa na waoneshaji kutoka nchi wanachama wa Jumuia hiyo ya Afrika Mashariki ilifanyika katika banda la Tanzania ambayo ndiyo nchi Mwenyekiti wa jumuia hiyo kwa sasa.

Akizungumza kwa niaba ya Jumuia hiyo, Waziri wa utalii wa Uganda Prof Epharaim Kamuntu amesema nchi zinazounda Jumuia hiyo zina vivutio vya utalii vya pekee na kuwataka watalii kuzitembelea nchi hizo huku akiwahakikishia kuwa eneo hilo la Afrika ni salama kabisa kwa watalii.

Mapema akiwakaribisha Mawaziri wa utalii na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk. Asha Rose Migiro amesema umoja na mshikamano wa nchi wanachama wa Jumuia hiyo umezidi kuimarika na kwamba miundo mbinu ya utalii katika nchi zote wanachma imeboreshwa sana na hivyo kuwafanya watalii kufurahia safari zao katika eneo hili la Afrika.

Maonesho ya WTM ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani baada ya yale ya ITB ya Ujerumani hufanyika kila mwaka mwezi Novemba nchini Uingereza ambapo mwaka huu yameanza Novemba 7 na yanatarajia kumalizika leo tarehe Novemba 9, 2016.

Katika maonesho ya mwaka huu makampuni 42 kutoka sekta binafsi na taasisi nne (4) za Serikali yanashiriki maonesho hayo chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania. Taasisi hizo za Serikali ni Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Bonde la Ngorngoro (NCAA) Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) na Bodi ya Utalii Tanzani (TTB).
Balozi wa Tz nchini Uingereza Dk.Asha Rose Migiro akiwakaribisha mawaziri na mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki kwenye banda la Tanzania wakati wa sherehe ya Jumuiya hiyo iliyofanyika jana katika banda la Tanzania.
Waziri wa utalii wa Uganda Prof Epharaim Kamuntu akitoa tamko (press statement) kwa niaba ya nchi zote za jumuiya Africa ili kuvutia watalii waweze kutembelea nchi za Afrika mashariki.
Washiriki toka sekta binafsi wakiwa kwenye maonesho ya utalii ya World Travel Market (WTM) katika banda la Tanzania chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania -TTB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...