Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TANZANIA yaendelea kusuasua katika soka na kushuka kwa nafasi 16 na kufikia nafasi ya 160 na 48 kwa Afrika huku Argentina wakiendelea kushika namba moja kidunia.
Viwango hivyo vya FIFA vimekuja baada ya michezo ya kirafiki iliyofanyika kuanzia Novemba 13-17 na Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki na Zimbabwe na kuambulia kufungwa goli 3-0.
Chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa timu ya Taifa imekuwa haina mafanikio kwa kushindwa kupanda au kupata matokeo mazuri kwa kucheza mechi 11, kushinda 1 kutoka sare tatu na kufungwa mechi saba.
Argentina licha ya kufungwa wameendelea kushika namba moja kidunia, Senegal wameshika nafasi ya 33 kidunia na namba moja kwa Afrika ikifuatiwa na Ivory Coast nafasi ya 34,Tunisia 35, Misri 35 na Algeria wakishika nafasi ya 38.
Nchi za Afrika zimeonekana kushindwa kufurukuta mbele dhidi ya matafifa ya Ulaya na America hasa baada ya kushindwa kuingiza timu kwenye timu 20 bora.
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani wameshushwa kwa nafasi moja mpaka nafasi ya tatu na Brazili kukaa nafasi ya pili.
Viwango vingine vya Fifa vitatolewa tena Desemba 22, 2016 - ambayo itatoa timu ya mwaka na mwanzilishi wa Mwaka.
msaada kutoka FIFA.COM RANKING
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...