THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANZIA: Balozi Waziri Juma afariki dunia, kuzikwa Alhamisi


Balozi mstaafu wa Tanzania nchini China na Sudan na mkuu wa mikoa mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza Balozi Waziri Juma (pichani) amefariki dunia jana jijini Dar es salaam alikopelekwa kwa matibabu.
Kwa mujibu wa binti yake Mwanamuziki Kida Waziri, mwili wa marehemu utasafirishwa leo  Jumatano kupelekwa Tanga kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi kijijini kwake Nairobi Jirihini kata ya Gombero Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga.
Innalillah Wa inna ilayh rajiun
Mola aiweke roho ya 
marehemu mahali pema peponi
- Amin,