CHAMA Cha waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepokea kwa masikitikio makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Said Muhammed Abeid,  kilichotokea  jana Novemba 7, 2016 alasiri katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

Atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na wanahabari na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo,  alikuwa kiungo kikubwa kwa TASWA kufanikisha matukio mbalimbali ya udhamini.

TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, klabu ya Azam na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha Mzee Said, huku tukiwatakia moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Itoshe kusema tumepoteza mtu muhimu sana, ambaye  mchango wake na uhodari havitasahaulika kwa wadau wa michezo.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...