Wabunge wa Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania ambao ni wanachama wa Timu ya Yanga, wamekutana leo mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu timu yao ikiwa ni pamoja na kuupata uongozi wa Tawi lao kwa muda huu wa mpito. Wabunge hao wanaYanga, wamefanikisha zoezi la kuchagua viongozi wa mpito wa Tawi lao.

Katika kikao hicho, Waliwachagua Mh. Venance Mwamoto (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Tawi hilo, huku nafasi ya umakamu ikishikwa na Mh. Ridhiwani Kikwete, Mh. Hafidh Ally Tahir -Katibu Mkuu, Mh. Hamidu Bobali -Naibu Katibu, Mh. Martha Mlata-Mweka Hazina na Mh. Abdallah Ulega anakuwa Mweka Hazina Msaidizi.

Kwa upande wa kamati tendaji, Wajumbe wake ni kama ifuatavyo. Mh. Grace Kihwelu, Mh. Halima Mdee, Mh. Seifu Gulamali, Mh. Gibson Meiseyeki, Mh. Issa Mangungu pamoja na Mh. Dotto Biteko

Katika Baraza la Wazee wa Yanga Bungeni, kuna Mh. Freeman Mbowe, Mh. Mwigulu Nchemba, Mh. Hawa Ghasia pamoja na mjumbe mmoja ambaye atatoka Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kweli Binaadam hamna kitu na duniani katu si pa kukaa milele. Inasikitisha sana na huzuni kubwa isiyomithilika. Marehem Hafidh Ali Tahir aliweza hata kuhudhuria kikao hicho cha Tawi la Yanga Bungeni na hata kupata wadhifa huo wa ukatibu Mkuu, lakini kama ndoto kufumba na kufumbuwa hata siku kamili haikutimia tunaskia keshakuwa marehemu. Ni vigumu kuamini khususan kama hukuwa umeishoma khabari hii mapema na kuja kuipitia wakati huu ambapo hilo la Manani limetokea, kwa kweli ni mshtuko na vigumu kuamini, lakini yote hiyo ni QADARI YAKE ALLAH, kwani kheri na shari zote hutokana na yeye Mwenyeez Mungu Mmoja. (Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiuna) Mola amughufirie kwa yote amjaaliye kauli thabiti na ampumzishe palipo pema peponi - AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...