Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi. Rosemary Msasi akongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani  ambapo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto kike na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani na kuwataka wanafunzi watakaotumia bweni hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu ili kuwawezesha wengine kulitumia.
 Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi akisoma taafifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wakike katika shule hiyo ikiwamo kusafiri umbali mrefu kuja shuleni.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa  anaamini lengo la mradi huo lenye dhumuni ya kumuendeleza mtoto wa kike litasaidia kuondo chagamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wa kike kwa muda mrefu.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi,walimu na viongozi wa mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.

(PICHA NA KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...