TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshukuru Umoja wa Mataifa kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa taasisi zisizo za kiserikali za kujengea uwezo wa kuweza kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay wakati wajumbe wa nchi za Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa programu za Umoja wa Mataifa zinazotekelezwa nchini Tanzania walipozuru katika ofisi hizo kwa mazungumzo.

“Kuna ongezeko kubwa la ufahamu kuhusu haki za binadamu, upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu, uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na kuboreshwa kwa huduma za kisheria na ukaribu wa serikali wa kufanyakazi na wadau wa haki za binadamu,” alisema Massay akifafanua zaidi kuhusu manufaa ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha haki za binadamu nchini.

Katika mazungumzo yao na ujumbe wa nchi za Nordic ambazo ni Sweden, Denmark, Norway Finland na Iceland kulikuwepo pia asasi mbalimbali zisizo za kiserikali kama Women’s Legal Aid Center, Tanzania Women Lawyers Association, Tanzania Women Judges Association, Legal Aid and Human Rights Center, Human Rights Defenders Coalition, na Tanganyika Law Society.

Katika mazungumzo hayo asasi hizo zilielezea ufanyaji kazi wao mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo na umuhimu wa ufadhili wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia changamoto zinazokabili Umoja wa Mataifa, serikali na asasi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema ipo haja ya kuwa na muono wa muda mrefu wa kuratibu shughuli zinazohusiana na maendeleo endelevu.



Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kushoto) akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam.

 Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na tume hiyo kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo.



Kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist (kulia) akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic ulipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...