Mshindi wa Jumla wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Juma likuli akiwa amenyenyua vikombe alivyokabidhiwa na Jaji Mkuu  Mh Othman Chande aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam.(
 Mshindi wa Kundi la Wanawake wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo  Sophia Mathias  akipokea zawadi ya Meza  aliyekabidhiwa na Mke wa Jenerali Mstaafu Waitara katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam.(
 Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Mawazo na wachezaji mwenzi ambaye ni katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (katikati) katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima.(
 Mwenyekiti wa  Klabu ya Lugalo brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwa ameshika zawadi ya kikombe alichokabidhiwa  na Chama cha Golf Tanzania TGU ikiwa ni ishara ya Kutambua Mchango wa Klabu hiyo katika kukuza mchezo wa Golf Nchini kulia ni mweka hazina wa TGU Akhil Yusuphali mara baada ya mashindano ya Waitara yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam
Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Matokeo na wachezaji wenzie,katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (kushoto)  na katibu mkuu wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima katikati katika mashindano ya Waitara Trophy  Jumamosi Novemba 19 jijini  Dar es salaam.(Picha zote na Luteni Selemani Semunyu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...