Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii
  Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Ubalozi wa china  hapa nchini ,imeandaa semina  kwa ajili ya jumuiya ya wafanyabiashara wa China kwa lengo la kuwaelimisha juu ya masuala mbalimbali ya ulipaji kodi.
  Semina hiyo inayotarajiwa kufanyika Novemba 25  katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), inatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Biashara na viwanda Mh. Charles Mwijage pamojana na Balozi wa China hapa nchini.
 
  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa walipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema, semina hiyo itawawezesha  wafanyabiashara wa china kutimiza na kuzingatia sheria za kutoza kodi sahihi na kukokotoa kodi ya Zuio katika bidhaa na huduma na hivyo kuongeza ulipaji kodi kwa hiari miongoni mwao.
  Kayombo amesema, katika semina hiyo mada mbalimbali zitawakilishwa zikiwa ni pamoja na Mabadiliko ya Bajeti ya 2016/17,Masuala ya Forodha na uondoshaji wa bidhaa, Kodi ya Zuio hususan katika sekta ya ujenzi na kodi ya Ajira, ambapo pia wafanyabiashara watapata fursa ya kuuliza maswali ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
 
  Kwa upande wake Mratibu  wa wafanyabiashara wa China, Andrew Huang amesema, Semina hiyo itawasaidia katika kuendelea kutekeleza wajibu wao na kuhakikisha wanalipa kodi inayostahili kutokana na shughuli zao wanazozifanya hapa nchini.
  "Tunashukuru sana TRA kwa kushirikiana nasi katika kutoaji wa elimu hii kwetu, kwani kwa kufanya hivyo ni dhahiri kwamba wanatukumbuka na kutujali nasi tutaonyesha ushirikiano kwa kuendelea kulipa kodi inayostahili."
  Ikiwa ni semina ya 15 tangu kuanza kwa semina kati ya mamlaka ya Mapato Tanzania na Ubalozi wa china,TRA imekuwa ikiendesha semina mbalimbali kwa wachina kuhusu masuala ya kodi kwa maombi au kutokana na mipango ya TRA kuelimisha makundi mbalimbali ya walipa kodi ili kuongeza uelewa wa Masuala ya Kodi hapa nchini.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa china itakayofanyika tarehe 25 Novemba 2016, leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jiteng Consultancy Limited Bw. Andrew Huong na Meneja Msaidizi wa Kampuni hiyo Bw. Wesley Huung (kushoto). Picha na Frank Shija – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...