Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeendelea kuonesha ubabe  kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika mashindano ya yanayoshirikisha Taasisi za Umma, baada ya kuichapa NSSF  kwa magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa katika kiwanja cha TPDC, Mikocheni.  
Kutokana na matokeo hayo, TTCL inaongoza kundi B baada ya kuvuna  pointi Tisa (9), katika michezo hiyo inayochezwa kila wikiendi. 
Ushindi huo dhidi ya NSSF ulishuhudiwa  pia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu,Waziri Kindamba aliyefika katika viwanja hivyo ili kuongeza nguvu kwa vijana wake wa TTCL. 
Mchezo ulikuwa Mkali kwa pande zote mbili, uku wakishambuliana kwa zamu, mpaka kipindi cha  kwanza kinakamilika timu zote zilikuwa bado hazijafungana. 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi  kwa pande zote mbili, magoli ya TTCL yalifungwa na  Peter Ntwala  na Raphael Ntila, uku bao machozi la NSSF lilifungwa na Iddi Rajibu.
Nahodha  wa TTCL, Samuel Uwiso na kocha Julius Kilenga wamesema kuwa siri ya ushindi unatokana na juhudi za wachezaji kuzingatia mazoezi na maelekezo kutoka kwa viongozi wao. 
Naye, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba amewapongeza wachezaji wa TTCL  kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuongoza kundi B, na kuwasihi wachezaji wasibwete na matokeo hayo bali iwe chachu ya kujiandaa na michezo mingine. 

TTCL inaongoza katika kundi B, ikifuatiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (NAOT) 
   Wachezaji wa TTCL na NSSF wakipeana mikono kabla ya mchezo huo kuanza, katika kiwanja cha TPDC

  Timu ya TTCl wakiwa katika picha ya pamoja

 Hatari katika lango la NSSF wakati TTCL wakipiga kona
 Walinzi wa TTCL wakithibiti mashambulizi ya NSSF

1.       Kaimu Afsa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw Waziri Waziri Kindamba (fulana nyeusi) akiwapongeza na wachezaji wa TTCL baada ya mechi kumalizika na ushindi wa Magoli 2 dhidi ya NSSF, katika kiwanja cha TPDC. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...