Jumla ya vijana 50 wameondoka nchini leo kuelekea China, kusomea kozi mbalimbali ikiwemo za afya na uhandisi katika masuala ya Petroli kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza masomo yatakayochukua miaka minne na sita kutegemea na aina ya kozi.
Wakizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kupaa kuelekea China, vijana hao wameelezea matumaini yao kuwa stadi na maarifa wanakayokwenda kupata nchini humo katika Shahada za Udaktari na Upasuaji, Uhandisi wa Masuala ya Petroli na Usanifu Majengo, vitakuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.
Thomas Macha na Sabir Abdulrahman, wanaokwenda katika vyuo vikuu vya majimbo ya Shenyang na  Hubei, wamezungumzia matarajio yao, wakiamini masomo wanayoenda kusoma yataisaidia Serikali kuelekea Tanzania ya Viwanda inayohubiriwa na Serikali ya Wamu ya Tano.
Miongoni mwa wasichana 20 kati ya vijana hao 50 wanaokwenda nchini humo, Monica Malugu na Anastacia Meresho, nao wamezunguzia matarajio yao ikiwemo mitazamo kuwa wanawake hawawezi masomo fulani kwa kuwa ni magumu.
Aidha, Glory Minja, mwakilisi wa Taasisi ya Universal Abroad Link (UAL), yenye dhamana ya kuwatafutia vyuo na ushauri kulingana na soko la ajira na kujiajiri, amesema,kila kitu kiko sawa na kwamba wanasubiriwa kuanza masomo.
 
Meneja wa Taasisi ya Universities Abroad Link (UAL), Joash Hosea akiagana na baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini China kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 50 wamekwenda China kwa ajili ya masomo ya Udaktari, Uhandisi pamoja na Mafuta na Gesi
Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini China wakimsikiliza Meneja wa Taasisi ya Universities Abroad Link, Joash Hosea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya wanafunzi 50 walikwenda China kwa ajili ya masomo ya Udaktari, Uhandisi pamoja na Mafuta na Gesi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...