THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISIWANI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Nd,Nassor Ali Nassor Mchoraji wa ramani katika kampuni ya United Construction LTD,(katikati) wakati alipotembelea jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni leo akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mikoa ya Pemba,(kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheir,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa madarasa mapya ya Maandalizi katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya Maendeleo.
 Wanafunzi wa Maandalizi wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein mara baada ya kuyazindua madarasa yao leo katika Skuli ya Gando Wilaya yaWete Mkoa wa Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya Maendeleo Kisiwani Pemba,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,hati maalum ya kukamilisha Ujenzi wa madarasa mapya ya Maandalizi yaliyojengwa kwa kupitia Tassaf katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo wakati wa Uzinduzi wa Rasmi wa Madarasa hayo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba ya ufunguzi wa jengo la madarasa mapya ya Maandalizi yaliyojengwa kwa kupitia Tassaf katika Skuli ya Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,(kulia)  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,na (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed.