THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UGENI WA NORDIC WATUA WIZARA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI

Serikali ya Tanzania imeshukuru msaada mkubwa unaotolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na mfumo imara wa utoaji haki kwa kuzingatia demokrasia na uwajibikaji.

Serikali imesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika mfumo ya utoaji haki nchini kutokana na misaada iliyotolewa na nchi hizo kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambao unasaidia mpango huo wa UNDAP.

Hayo yameelezwa wakati ujumbe mzito wa kutoka nchi za Nordic ulipotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria. Nchi hizo za Nordic pamoja kutoa mchango wake mkubwa katika bajeti za serikali ya Tanzania pia hutoa mchango mkubwa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake nchini.

Mataifa hayo ni ya Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland ambayo kwa pamoja yanaitwa mataifa ya Nordic ni wadau muhimu wa Umoja wa Mataifa na pia kwa serikali ya Tanzania.

Ujumbe kutoka nchi hizo upo nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano kati yao na Mashrika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyakazi kama taasisi moja na nchi hizo (Delivering as one) kwa lengo la kuimarisha na kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).Katika ziara hiyo iliyoanzia Novemba 14 wajumbe hao waliweza kuangalia utekelezaji mbalimbali wa miradi ya Umoja wa Mataifa na hasa hatua za mwanzo za miradi ya UNDAP ll.

Ujumbe huo wenye watu 13 kutoka Wizara za Mambo ya Nje za mataifa hayo wanatarajia kuzuru pia Kigoma na Dodoma wakimaliza Dar es Salaam.

Wakiwa Dar es Salaam, jana na leo watakutana na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na AZAKI na pia wanatarajia kutembelea ofisi za Bunge.Taarifa iliyotolewa katika mkutano huo imesema ingawa msaada wa Umoja wa Mataifa umekuwa siku zote ukililenga eneo maalumu linaloshughulikiwa na mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, imekuwa nguvu kupima athari zake katika maeneo mbalimbali yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo akielezea dhumuni la ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulipotembelea wizara wake jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.