Na Sekela Mwasubila 
Afisa habari, halmashauri ya wilaya ya ulanga

Mkuu wa wilaya ya Ulanga mh. Jacob Kassema amewaomba wakala wa misitu na wadau wengine wa elimu kuchangia ujenzi wa madarasa na upatikanaji wa madawati katika shule ya sekondari ulanga.

Aliyasema hayo wakati wa akipokea msaada wa madawati kutoka kwa wakala wamisitu wilayani ulanga ikiwa ni mchango wao wa kuunga mkono agizo la rais la kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati.

Alisema kuwa anawashukuru wadau hao kwa msaada wao mkubwa walioutoa kwaniutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la madawati ndani ya wilaya nakuongezea kuwa wasiishie hapo kwani bado kuna mahitaji ya ukamilishaji wamadarasa katika shule ya sekondari ya ulanga ili kuhakikisha wanafunzi wakidato cha kwanza wanapata mahali pa kusomea kwani kuna upungufu wamadawati na madarasa.

Aidha amesema kuwa pamoja na serikali kutenga fedha kwa ajili ya
ukamilishaji wa madarasa hayo lakini pia kama wadau wa maendeleo
wasichokekuchangia katika shule hiyo kwani maendeleo ya ulanga
yateletwa na wadau wamaendeleo.

Pia kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Ulanga bwana Yusuf Semuguruka aliongeza kwa kuwashukuru wadau hao kwa mchango wao na kusema kuwa msaada huo utaelekezwa katika shule ya
sekondari ulanga ilikuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza
wanakaa kwenye madawati.

Hata hivyo diwani wa kata ya mahenge mjini mh. nassoro kihiyo
aliwashukuruwadau hao kwa msaada huo na kusema kuwa kwa kushirikiana na madiwani wengine watahakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule yasekondari ulanga wataanza kidato cha kwanza na wote watakaa kwenye madawatikwa kushirikiana na wadau wengine.

Wakala wa misitu wilaya ya ulanga wametoa madawati themanini kwa ajili
yashule za sekondari na msingi ili kukabiliana na tatizo la upungufu
wamadawati na kutimiza agizo la rais wa jamuhuri wa muungano wa
tanzania lakuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Kulia Mh. Jacob Kassema akipokea
madawati kwa kaimu Meneja Misitu Wilaya ya Ulanga Bwana Fredrick Lohay katika viwanja vya Shule ya Msingi Mahenge Mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...