THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UMOJA wa waandishi habari wanawake Tanzania(WJT) wafanya ziara ya utalii wa ndani hifadhi ya taifa ya Saadan

Na Editha Karlo,Globu ya Jamii -Saadani

UMOJA wa waandishi habari wanawake Tanzania(WJT)wameanza ziara ya utalii wa ndani na ya kazi katika hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Ziara hiyo ya siku kumi iliyofadhiliwa na SHIRIKA la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)ambayo imehusisha wanahabari wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini wa vyombo mbalimbali wanavyofanyia kazi.

Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa umoja huo wa wanahabari wanawake Ester Macha mwandishi wa gazeti la majira kutoka Mkoa wa Mbeya alisema kuwa ziara hiyo itawapa fursa ya kujifunza na kuona kwa vitendo vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi za Taifa watakazo tembelea.

"Tumefurahi sana ka wanahabari kupata fursa hii ya kutembelea hifadhi zetu ikiwa ni sambamba na kuzitangaza kupitia kalamu zetu"alisema Ester.Aliwataka wananchi wote kujenga tabia ya kutembelea hifadhi zetu nasi kuwaachia wageni kutoka nje peke yao kuja kutembelea hifadhi na kufanya utalii.

Naye Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Saadani Hapaikunda Mungure alisema hifadhi ya saadani ina utalii wa kuangalia wanyama kwa kutembea na magari,fukwe nzuri za bahari,utalii wa boti kwenye mto wami,matembezi ya miguu.
Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Saadani Apaikunda Mungure akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wa habari wanawake kuhusu utalii wa boti unaofanywa ndani ya mto wa wami katika hifadhi ya saadani.

Mwandishi wa habari wa blog hii Editha Karlo(kushoto)kutoka Kigoma na mwandishi wa gazeti la mwananchi Joyce Joliga kutoka Mkoa wa Ruvuma wakifanya utalii wa boti ndani ya mto wami uliopo hifadhi ya Taifa ya saadani.
Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa na vyombo mbalimbali wakifanya utalii wa ndani wa boti kati mto wami ndani ya hifadhi ya Saadani