THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UWEKEZAJI WA TANESCO WAFIKIA SHILINGI TRILIONI 5.35, NI MKUBWA KATIKA HISTORIA YA UMEME NCHINI

SERIKALI kupitia Shirika lake la umeme nchini TANESCO limefanya uwekezaji mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni 5.35, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016.

Akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika hilo, Mhandisi Mramba alisema, “Katika historia ya sekta ya umeme, haijawahi kutokea uwekezaji mkubwa kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi yote ya umeme inayoendelea na ambayo tayari iemtengewa fedha ina thamani ya Shilingi Trilioni 3.85, na majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi Mramba.

“ Uwekezaji huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.

Mhandisi Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania, TEDAP, Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi na Rusumo Power Plant (T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi kuhusu masuala muhimu ya TANESCO. Wengine pichani, kulia ni Meneja wa Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano wa Shirika hilo, Leila Muhaji.NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA